“Watu wengi waliomwamini Mtume Muhammad (SAW) walikuwa ni wale walioathiriwa na tabia na hulka yake njema; bila shaka, baadhi ya watu pia waliathiriwa na uthibitisho na hoja, lakini ni kawaida kwamba watu wengi wanavutiwa na kitu kwa sababu ya sifa zake za kimaadili,” Hujjatul Islam Mojtaba Kalbasi, mhadhiri mwandamizi katika Seminari ya Qom, ameliambia Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani, IQNA.
Alibainisha kwamba Qur'ani Tukufu inatumia usemi "usio wa kawaida" kuhusiana na Mtume Muhammad (SAW) pale inaposema, " Na hakika wewe una tabia tukufu." (Surah Al-Qalam, aya ya 4)
Neno 'tabia tukufu' katika Qur'ani linatumika katika mazingira kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuelezea tabia ya Mtume (SAW), ambayo inaakisi ukuu wa utu wake, alisisitiza Khatibu huyo .
Hapana shaka kwamba maingiliano ya Mtume (SAW) hata na waabudu masanamu na wale walioua makundi ya Waislamu wakati wa vita na migogoro, yaliegemezwa kwenye maadili ya Kiislamu na kiutu, Kalbasi aliongeza, pia akinukuu aya nyingine ya Quran Tukufu, “Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia." (Surah Al-Imran, aya ya 159)
"Tabia yake ya huruma na mwongozo ilikuwepo hata katika vita, na siku zote alijaribu kuepusha migogoro isipokuwa adui angeingia kwenye uwanja wa vita na panga na nia ya kuua, katika hali ambayo hapakuwa na chaguo ila kupigana," alisema.
Sira ya Mtukufu Mtume (SAW) na yale yaliyotajwa ndani ya Qur'ani Tukufu yanabainisha viwango vyake vya "kipekee" vya kimaadili, kwa mujibu wa mtafiti huyo.
Mtume Muhammad (SAW) hakulazimisha mtu yeyote kuukubali Uislamu, Kalbasi alisisitiza.
"Malezi na mwaliko wa imani hutofautiana na dhana zingine, na bila maadili, hazielekei popote. Mtume (SAW) alikuwa ni muongozo na mwalimu wa wanadamu, akiwafundisha hekima na Qur’ani,” alisema mwanazuoni huyo.
"Msingi ni mwaliko kwa Mungu, utu wa kibinadamu na kimungu, na mwinuko wa kiroho, na mwinuko huu hauwezi kufikiwa bila maadili," aliongeza.
3489749